Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika kipindi cha uongozi na uwelekezaji wa Imam Khamenei Shahidi, mojawapo ya maneno muhimu yaliyokuwa yakisisitizwa na mtu huyu wa Mwenyezi Mungu pamoja na kiongozi mwenye hekima na busara ni suala la “kujiamini kitaifa” na kufanya juhudi katika njia ya kujiimarisha, kwa mtazamo wake, kipengele hiki ni injini ya maendeleo na uti wa mgongo wa uhuru na heshima ya taifa letu katika nyanja mbalimbali.
Kwa mtazamo wa Imam na Kiongozi wetu Shahidi, kujiamini kitaifa kunamaanisha imani ya dhati ya moyo ya taifa katika kauli kwamba: “Sisi tunaweza,” hakika kwa kutimia kauli hii, pamoja na kudhoofisha vita vya kisaikolojia vya adui, tutashuhudia kustawi zaidi kwa uwezo na vipaji vya kitaifa katika nyanja mbalimbali, na kwa namna hiyo misingi ya maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia itaandaliwa vizuri nchini.
Kuhuisha hali ya Kujiamini kwa Taifa
Dk. Hamidreza Yazdani, mjumbe wa jopo la walimu wa Kitivo cha Farabi cha Chuo Kikuu cha Tehran, kuhusiana na suala hili alisema:
“Miongoni mwa athari na baraka za mwenendo, maneno na miongozo ya Imam na Kiongozi wetu Shahidi ni kwamba, katika miongo ya hivi karibuni, kwa maana halisi ya neno, kujiamini kwa taifa limehuishwa nchini mwetu.”
Pia, akirejelea msisitizo na matakwa maalumu ya Imam Khamenei Shahidi kuhusu kutekelezwa kwa harakati za uzalishaji wa elimu na mapinduzi ya kielimu nchini, alisema: “Kimsingi, mojawapo ya sifa muhimu zaidi za kipindi cha uongozi wake ni juhudi za pande zote za kubadilisha elimu kuwa nguvu na uwezo wa taifa; jambo ambalo tunaliona katika dhana pana ya uzalishaji wa elimu na harakati za kielimu.”
Harakati Kubwa ya Iran ya Kiislamu Katika Njia ya Maendeleo ya Kisayansi
Aliongeza kusema: “Katika kipindi hiki, kulikuwa na mkazo maalumu katika kubadilisha nafasi ya Iran kutoka kuwa mtumiaji wa elimu kwenda kuwa mtengenezaji wa elimu, harakati hii ilianza kwa kuwekeza katika taaluma zinazohesabiwa kuwa ‘kilele cha teknolojia’ kama vile sayansi zinazohusiana na nanoteknolojia, nishati ya nyuklia na seli shina, lengo kuu lilikuwa ni kwamba; Iran isiwe na haja ya kupata ruhusa au msaada kutoka kwa madola ya kigeni kwa ajili ya maendeleo yake.”
Yazdani pia alisema: “Kipengele kingine muhimu katika kipindi cha uongozi na usimamizi wa Imam Khamenei kinahusiana na suala la kujenga ukuta wa usalama (uwezo wa kumzuia adui kushambulia), maana yake ni kwamba; Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika miaka hii ilijenga mkakati wake wa ulinzi kwa msingi wa kuondoa vitisho mbali na mipaka yake.
Katika mwelekeo huu, kwa kuendeleza uwezo wa makombora na ndege zisizo na rubani na kwa kuunga mkono makundi yanayoshabihiana nayo katika eneo, iliundwa aina ya nguvu ya kuzuia ambayo ilifanya gharama ya shambulio lolote la kijeshi dhidi ya Iran kuwa kubwa sana kwa maadui, jambo hili pia lilisababisha uthabiti wa ndani wa usalama, na sehemu ya athari zake tumezishuhudia katika vita vya kulazimishwa vya siku kumi na mbili na hasa katika Vita vya Ramadhani.”
Kuwezesha Uchumi wa Ustahimilivu kwa Kusisitiza Elimu ya Kizazi cha Vijana
Akiendelea kusema, alisisitiza juhudi zisizochoka za kufanikisha uhuru wa kiuchumi kwa kutegemea kipengele cha ustahimilivu na kuongeza: “Msisitizo wa Kiongozi wetu Shahidi juu ya dhana ya uchumi wa ustahimilivu kwa lugha rahisi unamaanisha kujenga uchumi ambao hautaporomoka kwa sababu ya vikwazo na mashinikizo ya nje.
Jambo hili lilifuatiliwa kupitia kuunga mkono bidhaa za ndani, kupanua kampuni za maarifa na teknolojia, na pia kufanya juhudi za kubadilisha utegemezi kamili wa mapato ya mafuta kwa kuongeza mauzo ya nje yasiyotokana na mafuta.”
Mjumbe wa jopo la walimu wa Chuo Kikuu cha Tehran alikumbusha kuwa: “Suala lingine muhimu linahusiana na kufufua utambulisho wa kitaifa na Kiislamu, jambo ambalo Imam na Kiongozi wetu Shahidi walisisitiza sana. Kwa hakika, kwa mtazamo wa kitamaduni, mkazo mkuu ulikuwa juu ya kusimama dhidi ya mtindo wa maisha wa Kimagharibi na kurejea katika maadili ya asili na ya kidini, sifa hii ililenga kujenga jamii yenye kujiamini kitaifa ambayo hupata mfano wake wa maendeleo si kutoka Magharibi, bali kutoka katika mizizi yake ya kihistoria na kidini.”
Ulazima wa Kufafanua Njia ya Uongozi wa Kiongozi Shahidi na Wataalamu
Alisema: “Aina ya uongozi, maneno na miongozo ya Imam wetu Shahidi ilikuwa sababu ya kufufuliwa kwa kujiamini kitaifa, jambo ambalo rafiki na maadui wote wanakiri, ni lazima vipengele mbalimbali vya mafanikio haya vichambuliwe na kufafanuliwa kwa undani na wataalamu.”
Yazdani pia aliongeza: “Kwa ufupi, ikiwa tunataka kufupisha kipindi hiki katika sentensi moja, sifa yake kuu ni kujenga nguvu huru katika dunia yenye mihimili mingi ya nguvu.
Kwa hakika, mtindo huu wa utawala umejaribu kuonesha kwamba; nchi inaweza kufikia teknolojia za hali ya juu na kulinda usalama wake bila kujiingiza katika mfumo wa dunia unaotawaliwa na Magharibi, muhimu ni kwamba njia hii ifuatwe kwa nguvu na vijana, wanasayansi, walimu na maafisa ili tufikie malengo yote yaliyowekwa katika nyaraka za juu za taifa.”
Maoni yako